KUMPENDA
MUNGU
Hiki ndicho kitu ambacho Mungu anakitaka kiwe kwa
mtu anaye mwamini na kusema kuwa anaishi kwa matakwa ya Mungu, ili ni jambo
ambalo mtu yeyote anapotambua kuwa unampenda basi mtu huyo uwa na furaha na
wewe na nivigumu kukuacha kirahisi kirahisi tu.
Ni jambo linaloleta furaha kwa Mungu anapotambua
unafanya yote kwake kwa sababu moja tu kuwa UNAMPENDA. Hakuna jambo lolote
unaweza kumfanyia Mungu likambariki mbali na kumpenda hata yawe mambo ambayo
watu watakuogopa au kukuheshimu kwa
mambo makubwa unayo yafanya mathalani utoaji,kuomba,kuhubiri hama kutoa
unabii.( tendo lolote lisiloambatana na pendo kwa Mungu alina kibali machoni pa
Mungu).
Hata katika hali ya kibinadamu unaweza kufanya jambo
lolote kwa mtu hata ukimpa mtu madini “Tanzanite” kwa binadamu mwenye akili
timamu akigundua hii zawadi haijatoka katika moyo wa kunipenda hawezi kupokea
hiyo zawadi.
Moja ya jambo gumu katika kumpenda Mungu ni namna
gani nampenda Mungu kwa wakati gani na katika matendo yapi kwa maana Mungu
haonekani kwa macho haya ya nyama, kwakua kwa upande wa kibinadamu mtu
unayempenda au anaye kupenda utauona katika udhihirisho wa upendo wake na hapo
inakuwa katika nafasi ya kutambua nafanya nini katika hili.
Japo Mungu haonekani kwa macho haya ya nyama lakini
kumpenda hakupo katika hali ya kufikirika bali hali inayohusisha hisia
zako,hali ya moyo wako inabeba pendo la Mungu, ukweli kwamba huwa atumpendi
Mungu kwasababu tu alitupenda bali wajibu wetu kwake kumpenda yeye ilituweze kutenda wajibu wake kwetu katika
hali ya kumpenda.
Mungu afurahi sana kwakua unatumika bali unampenda
ndomana unamtumikia katika hali stahiki kwa furaha,kumpenda Mungu sio vile watu
wanavyompenda bal ni vile anavyotaka umpende kwa namna yake hakuna namna moja
ya kumpenda Mungu kutoka kwa mtu mathalani mtu anakesha sana katika maombi
basin awe ukaamua kukesha katika maombi ukijua huku ndiko kumpenda Mungu.
Napenda kusema kuwa ni rahisi sana kumpenda Mungu
kwa nafasi yako au mtazamo wako lakini ni ngumu sana kumpenda kwa matakwa yake.
Kumpenda Mungu ni tofauti kabisa na kumpenda mtu
yeyote au kitu chochote hivyo kumpenda Mungu ni uwanja mpana sana na wala sio
wakufikia hatua ya kusema kuwa mimi nampenda sana Mungu kwakua nafanya hili au
lile utakuwa unajidanganya mwenyewe.
Warumi 8:35,37 na 39
Nini
maana ya kumpenda Mungu?
Japo ziko maana nyingi ambazo watumishi pamoja na
wanajamii wakizungumzia juu ya kumpenda Mungu wapo wanasema kumpenda Mungu ni
kuhika neno la Mungu, wengine wanasema ni kutenda matendo ambayo Mungu
atayafurahia na wengine wanasema ni kuwatendea mema binadamu wenzako napia wapo
wanaosema kujali yatima na wajane….
KUMPENDA MUNGU ni
hali ya siri za Mungu zinapatikana tu kwa wenye kumkubali Roho mtakatifu na
kukubali kuingia gharama yeyote ili mradi tu yale ya Roho mtakatifu kupata
nafasi ndani yako(kufanyia kazi).
Japo katika katika kitabu cha yohana 14:23…yesu
akajibu,akamwambia,mtu akinipenda, atalishika neno la Mungu; na baba yangu
atampenda; nasi tutakuja kwake na kufanya makao kwake , na kufanya makao kwake.
-swala kubwa nalishikaje neno la Mungu je! Kwaku
lisoma tu na kulitendea kazi kwa namna ipi?
Zaburi 119:61,72 na 77
Warumi 8:28
Warumi 5:5
Yohana 14:23-24
Mathayo 12:31-32
Roho mtakatifu ni wa muhimu sana na hivyo kupitia
huyo anaweza kukusaidia kukufanya yale Mungu anayotaka kwa ufasaha zaidi na
pasipo huyo hakuna kumpenda Mungu kwakua ni yeye ajuaye namna gani Mungu
anavyotaka kupendwa.
1 wakorintho 2: 9-10
Jambo lolote unaloweza kulifanya nje ya muambatano
na Roho mtakatifu aliwezi kupata kibali kwa Mungu.
Mungu hataweza kukupenda wewe au pendo lako
alitafika kwake(Mungu) ila tu umekubali kufanyika kuwa mwana wa Mungu.
Yohana 1:12,15
Hili ni jambo ambalo Mungu analipenda kama kupendwa
katika moyo wa kweli katika mwenendo mzima wa maisha yako.
Mithali 8:17
Unapoanza kumpenda Mungu (kumcha) anaanza
kushughulika nawe katika kila kona ya maisha yako.
Mwanzo 15:15
Wakolosai 3:3
Mithali 10:27
Waamuzi 8:32
Yoshua 14:11
1 Nyakati 15:2(b)
Warumi 1:28
Katika yote ni vizuri kutambua kuwa kama usipo
mpenda Mungu katika kweli Mungu hawezi kukupenda…yohana 14:24,
Anza kumpenda Mungu kwanza kisha fanya yale
yanamuhusu Mungu kwa ukamilifu ndipo hapo kila tendo litapata kibali kwa Mungu.
Torati 30:15-16
MPENDE AKUPENDE KWA AJILI YA
FAIDA YAKE MUACHE
HAKUACHE KWA HASARA YAKO,
*kama ukimpenda ni wazi utamsikiliza kwa kupenda.
Prepared by ;