Alhamisi, 17 Oktoba 2013

KIJANA KATIKA KUJIKOMBOA



KIJANA  NI  NANI  NA  AFANYE  YA PI  ILI  KUJIKOMBOA?
 
Kijana ni hatua ya kujivunia sana kwani ni wakati wa kutambua na kuona mwanga sahihi wa maisha na kutambua kwanini upo na unahitaji nini ili uweze kuwa wa maana zaidi sana. Tuta kwenda kuangalia kwa namna ambayo itatusaidia kujitambua kuwa kijana ni nani na kuanza sawasawa na ulivyoelewa kwa pamoja tukielimishana tunaweza kufika mahali pa juu zaidi ambapo tunaweza kung’ara.

Ujana ni bidhaa adimu sana na ghali sana kwakua haiko hatua ambayo unaweza kuilinganisha na hatua hii kwakua ni ya kipekee na yatofauti sana.

Kijana ni nani?

Yoshua 21:18

kutokana na takwimu na maelezo ya watu mbalimbali wamejaribu kuelezea maana ya kijana katika namna mbalimbali mathalani muonekano wa kijana, nguvu katika utendaji, mawazo ya kijana na uchumi wa mtu aliye kijana na hata matumizi wa huo uchumi wa mtu huyo anaitwa kijana.

Kutokana na maelezo hayo mbalimbali lakini mimi nitajikita katika umri ambao tunaweza kupata maana ya kijana ni mtu aliye na umri ulioanzia 18 hadi 45 ni hatua ya kati kutoka utoto kwenda utu uzima.

Kijana kama kijana jua kwamba unalokusudi ambalo linabidi utoke na kwenda kwa jamii kubwa nao kupata kitu ambacho kitawafanya wa kukumbuke na waone fahari ya wewe kuwa pamoja nao.

Vijina katika dunia tuliyonayo ndio wanaoshangaza ulimwengu na kuufanya vile wanavyo taka wako vijana wengi wamejiingiza katika biashara ya madawa ya kulevya na wengine kujiingiza katika vitendo vya ngono katika kujirahishia maisha yao na wengine kufanya vitendo vya uhalifu kama vile ubakaji,wizi(ujambazi) na hata wengine kushiki katika kujitoa mwanga kuwatayari kujitoa kwa ajili ya maisha yao na mengine mengi ambayo vijana wamejiingiza katika hayo na hatimaye kupelekea kuwa katika majanga mbalimbali kama vile kifo.

Dunia ya sasa hakuna mitu mzuri ambaye anatafutwa kwa hali na mali kama kijana kwakua imefika nyakati kusema kwamba dunia ndio muhimiri wa dunia kupitia hao wanaweza kuifanya dunia kuwa katika hali tofauti ambayo watakayoikusudia katika hali njema au mbaya inawategemea wao.

Imekuwa ni kilio cha watu wengi hasa wazee kwa kuona vijana wanaangamia katika majanga yanayoikabili dunia ya sasa imekuwa zaidi ya tatizo kwakua kila majanga yanayotokea basi lazima kwa kiasi kikubwa wahusishwe watu ambao hasa  ni vijana ingawa kwa kiasi kikubwa hili kundi la vijana halifaidiki ipasavyo lakini linatumika sana huku likiendelea kuteketea.

Kusema ukweli kilio hiki sio cha wazazi au wazee tu bali hata Mungu mwenyewe ni anasikia maumivu makubwa kutikana hile hazina iliyo ndani ya mwanadam ambayo aliiweka mwenyewe kwa ajili ya kusudi lake lakini matokeo yake ile hazina inatumika kwa ajili kuubomoa ule ufalme wake anakosa furaha ya kujivunia vijana ambayo walitakiwa wabebe sura yake,nguvu zake,mmlaka yake hapa duniani kwa kufanya yaliyo yake.

Japo katika hali hii utaitole hesabu ya nguvu na uwezo binafsi aliyokupa Mungu umeitumiaje wakati ambao hakuta kuwa na wakati wakurudi nyuma tena.

I saya 47:8-11,15

I wakorintho 7:32

Maombolezo 3:27

Vijana wengi wamepotelea katika maisha ambayo hatima yake ni kupotea kabisa pasipo matumaini mema mbayo Mungu alikusudia ndani ya neno lake Mungu anasema kwamba afurahishwi na kifo cha mwenye dhmbi, kwakua hana matarajio mabaya kwa mwanadamu yeyote mbaye yeye Mungu alimkusudia.

Ezekieli 33:11
   
  “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi,asema BWANA , ni mawazo ya amani wala sio mabaya kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.”

Yeremia 29:11

Mungu ajaweka jehanamu kwa ajili ya kuangamiza maisha ya mwanadamu bali ilikuwa ni kwa ajili ya shetani na malaika wote walio muasi na sio kwa ajili ya mwanadamu hivyo Mungu umia sana kuona watu wakienenda na hatima yao kuwa sawa na shetani anapokwenda.

Japo kuna maneno ambayo wanadamu wanasema kuwa Mungu ametuacha ukweli ni kwamba ni sisi ndio tulio muacha Mungu kwakujua au kutokujua.

Mungu akumtengeza kijana kwa namna alivyo kwa kusudi kwamba aje ateseke naye Mungu afurahie kwa kuteseka kwako kamwe hilo silo kusudi la Mungu lisivyokuwa kusudi la mzazi kwa mwanae aliye mzaa.
Katika hali ya uhalisia ni kweli kwamba sio utoto au ujana wala utuuzima waeza kukuwezesha uweze kufanya upasavyo bali ni Mungu tu ndani yako akuwezeshe WOKOVU  HALISI.

Yohana 15:5

Ukweli utakapo ujenga ujana katika misingi mizuri ni wazi hapo ndipo utaona ustawi mzuri wa Ki Mungu ndani ya hatua zinazofuata pasipo upingamizi wowote utakao kushinda bali vyote vinakuwa ni rahisi kufanyika kwa Mungu anatembea kupitia wewe.

Na ndipo hapo utaweza kustarehe katika ujana wako na kufurahia maisha yako yote kwakua furaha yako itakuwa ikilindwa na Mungu.

Yohana 21:18

Ujana ni hatua ambayo akili inapevuka na kuuhitaji kujua vitu vingi na vitu vingine ambavyo alikuwa mwanzo anakosa uhuru kuvijua basi tumia fursa hiyo kujua zaidi sana kuhusu Mungu ili upone na dunia hii iliyojaa kila haina ya matatizo.

Wakolosai 2:23

Yeremia 3:4-5



Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                   
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com





Ni vizuri tuseme kuwa tunakupenda……………siku njema!!


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni