Ijumaa, 27 Desemba 2013

UJANA ULIO SALAMA



KANUNI  ZA  KUTUNZA  UJANA  WAKO;

Ujana kama lulu ambayo inathamani kubwa sana katika dunia ya sasa hivyo inahitajika sana kutunzwa ili iweze kuendelea kuwa bora sana na yenye manufaa katika kizazi chote. Kama inavyojulikana wazi kitu chochote kisipotunzwa basi kunahali ya kuharibika ambayo inakaribia na isipoangaliwa jambo baya linaweza kupelekea kutia nanga katika ujana.

Jua kama usipo jitambua na kujithamini hakuna mtu atachukua nafasi yako na kufanya yale uliyotakiwa kujifanyia wewe binafsi.

Unaweza kutamani kuwa kijana unaye jitunza lakini usipofuata kanuni ambazo zinazo kuwezesha kujitunza hauwezi kuwa kijana wa maana kwa Mungu na kwa wanadamu na hatimae dunia ikafaidika kupitia wewe.

Kila namna unatamani kuwa lazima pawepo na namna ya kukufanya wewe kuwa mtu husika mathalani ukita kuwa mwalimu mzuri kuna kanuni za kukufanya uwe hivyo na vilevile ukitaka kuwa mwanafunzi bora lazima kuna kanuni/namna ya kukufanya mwanafunzi bora unaweza ukatamani kuwa mtu yeyote kwa namna ya mtazamo wako ulivyo lakini kama ujafuata kanuni zilizowekwa kamwe hauwezi kuwa vile unatamani.

Hivyo unaweza kutamani sana lakini kama tu hautafwata kanuni kamwe hauwezi kufika pale unafikiria hivyo
 KUTAMANI  BILA  KUFUATA  KANUNI  HAKUNA  KITU KITAKACHOFANYIKA.

Kanuni za kutunza ujana wako katika kiwango cha Mungu;

i.kumpenda Mungu

ii.pendo la Mungu kuchukua nafasi ndani yako

iii.usiogope

iv.macho ya rohoni

v.ukaribu

vi.kumtazama Mungu

vii.kujitunza

viii.uaminifu

ix.usijiamini

x.maongezi


Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                   
                     Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com             

Ijumaa, 6 Desemba 2013

NAMPENDAJE MUNGU?



KUMPENDA   MUNGU

Hiki ndicho kitu ambacho Mungu anakitaka kiwe kwa mtu anaye mwamini na kusema kuwa anaishi kwa matakwa ya Mungu, ili ni jambo ambalo mtu yeyote anapotambua kuwa unampenda basi mtu huyo uwa na furaha na wewe na nivigumu kukuacha kirahisi kirahisi tu.

Ni jambo linaloleta furaha kwa Mungu anapotambua unafanya yote kwake kwa sababu moja tu kuwa UNAMPENDA. Hakuna jambo lolote unaweza kumfanyia Mungu likambariki mbali na kumpenda hata yawe mambo ambayo watu  watakuogopa au kukuheshimu kwa mambo makubwa unayo yafanya mathalani utoaji,kuomba,kuhubiri hama kutoa unabii.( tendo lolote lisiloambatana na pendo kwa Mungu alina kibali machoni pa Mungu).

Hata katika hali ya kibinadamu unaweza kufanya jambo lolote kwa mtu hata ukimpa mtu madini “Tanzanite” kwa binadamu mwenye akili timamu akigundua hii zawadi haijatoka katika moyo wa kunipenda hawezi kupokea hiyo zawadi.

Moja ya jambo gumu katika kumpenda Mungu ni namna gani nampenda Mungu kwa wakati gani na katika matendo yapi kwa maana Mungu haonekani kwa macho haya ya nyama, kwakua kwa upande wa kibinadamu mtu unayempenda au anaye kupenda utauona katika udhihirisho wa upendo wake na hapo inakuwa katika nafasi ya kutambua nafanya nini katika hili.

Japo Mungu haonekani kwa macho haya ya nyama lakini kumpenda hakupo katika hali ya kufikirika bali hali inayohusisha hisia zako,hali ya moyo wako inabeba pendo la Mungu, ukweli kwamba huwa atumpendi Mungu kwasababu tu alitupenda bali wajibu wetu kwake kumpenda yeye  ilituweze kutenda wajibu wake kwetu katika hali ya kumpenda.

Mungu afurahi sana kwakua unatumika bali unampenda ndomana unamtumikia katika hali stahiki kwa furaha,kumpenda Mungu sio vile watu wanavyompenda bal ni vile anavyotaka umpende kwa namna yake hakuna namna moja ya kumpenda Mungu kutoka kwa mtu mathalani mtu anakesha sana katika maombi basin awe ukaamua kukesha katika maombi ukijua huku ndiko kumpenda Mungu.

Napenda kusema kuwa ni rahisi sana kumpenda Mungu kwa nafasi yako au mtazamo wako lakini ni ngumu sana kumpenda kwa matakwa yake.

Kumpenda Mungu ni tofauti kabisa na kumpenda mtu yeyote au kitu chochote hivyo kumpenda Mungu ni uwanja mpana sana na wala sio wakufikia hatua ya kusema kuwa mimi nampenda sana Mungu kwakua nafanya hili au lile utakuwa unajidanganya mwenyewe.

Warumi 8:35,37 na 39


Nini maana ya kumpenda Mungu?

Japo ziko maana nyingi ambazo watumishi pamoja na wanajamii wakizungumzia juu ya kumpenda Mungu wapo wanasema kumpenda Mungu ni kuhika neno la Mungu, wengine wanasema ni kutenda matendo ambayo Mungu atayafurahia na wengine wanasema ni kuwatendea mema binadamu wenzako napia wapo wanaosema kujali yatima na wajane….

KUMPENDA MUNGU ni hali ya siri za Mungu zinapatikana tu kwa wenye kumkubali Roho mtakatifu na kukubali kuingia gharama yeyote ili mradi tu yale ya Roho mtakatifu kupata nafasi ndani yako(kufanyia kazi).

Japo katika katika kitabu cha yohana 14:23…yesu akajibu,akamwambia,mtu akinipenda, atalishika neno la Mungu; na baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake na kufanya makao kwake , na kufanya makao kwake.

-swala kubwa nalishikaje neno la Mungu je! Kwaku lisoma tu na kulitendea kazi kwa namna ipi?

Zaburi 119:61,72 na 77

Warumi 8:28

Warumi 5:5

Yohana 14:23-24

Mathayo 12:31-32

Roho mtakatifu ni wa muhimu sana na hivyo kupitia huyo anaweza kukusaidia kukufanya yale Mungu anayotaka kwa ufasaha zaidi na pasipo huyo hakuna kumpenda Mungu kwakua ni yeye ajuaye namna gani Mungu anavyotaka kupendwa.

1 wakorintho 2: 9-10

Jambo lolote unaloweza kulifanya nje ya muambatano na Roho mtakatifu aliwezi kupata kibali kwa Mungu.
Mungu hataweza kukupenda wewe au pendo lako alitafika kwake(Mungu) ila tu umekubali kufanyika kuwa mwana wa Mungu.

Yohana 1:12,15

Hili ni jambo ambalo Mungu analipenda kama kupendwa katika moyo wa kweli katika mwenendo mzima wa maisha yako.

Mithali 8:17

Unapoanza kumpenda Mungu (kumcha) anaanza kushughulika nawe katika kila kona ya maisha yako.

Mwanzo 15:15

Wakolosai 3:3

Mithali 10:27

Waamuzi 8:32

Yoshua 14:11

1 Nyakati 15:2(b)

Warumi 1:28

Katika yote ni vizuri kutambua kuwa kama usipo mpenda Mungu katika kweli Mungu hawezi kukupenda…yohana 14:24,

Anza kumpenda Mungu kwanza kisha fanya yale yanamuhusu Mungu kwa ukamilifu ndipo hapo kila tendo litapata kibali kwa Mungu.

Torati 30:15-16

MPENDE  AKUPENDE  KWA  AJILI  YA  FAIDA  YAKE  MUACHE  HAKUACHE KWA  HASARA  YAKO,

*kama ukimpenda ni wazi utamsikiliza kwa kupenda.

Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com