Jumanne, 27 Agosti 2013

je! mavazi yana nafasi gani katika ukristo



                                                             MAVAZI;
 
Mavazi ni gumzo katika jamii yetu tuliyonayo imeathiri heshima ya mtu kwa aliye muhusika,Yule aliye vaa vizuri basi uheshimiwa kutokana na muonekano na alivaa isivyo onekana vyema basi heshima kwa mtu huyo upotea.
Wako watu wanakosa uhuru kutokana na hali hii, je! Vazi sahihi kwa mtu ni lipi na kwanini likawa lile na lisiwe hili.
Jambao hili limekuwa ni tatizo ikitegemea na familia husika au jamii husika kwa wakati familia moja inatoa ruhusa juu ya vazi Fulani na jamii nyingine inakataza. Hivyo hali hii inategemea jamii husika kwakua ndani ya jamii kuna mgawanyiko wapo wana wanakubali na jamii nyingine hawakubali.
Wako watu ambao wametengwa na jamii katika huduma kama vile kanisani,hospitali na maeneo mengine kwa sababu ya mavazi.


Katika kujadili jambo hili yako mambo inabidi tuyaangalie:
                               (a)Je! Nguo inawezekana kuwa tatizo katika ukristo.
                               (b)Je! Nguo inamchango wowote katika kufanya ibada.
                             (c)unafikiri Nguo inaweza kutoa picha ya mkristo(ushuhuda) kwa waliookoka na wasio okoka.
          Katika kuangalia kwa utangulizi tatizo linaweza kuwa pande zote mbili kutokana na mitazamo tofauti iliyoko ndani ya jamii yetu,
-kwa nini mtu binafsi ameamua kuvaa(msukumo gani umepelekea kuvaa vile ulivyo vaa) na anayekutazama kwa nini amefikia hapo(mtazamo gani aliokuwa nao ikampa tafsiri hiyo ambayo mtu binafsi ameiamini)
2 samweli 13:18
Ni kweli Mungu ashughuliki na muonekano wanje bali NIA YAKO katika muonekano wako. Hiyo  inawezekana hali hiyo kuwa shida kwa jamii lakini si kwa Mungu, kwakua muonekano wako haumbadilishi Mungu mtazmo wake kwako  bali inaweza kuwa najisi kwa watu.
Ni kweli unaweza kuvaa vizuri katika muonekano wowote lakini bado usiwe ushuhuda mzuri kwa jamii japo katika hali hii bado hatuamasishi kuvaa kwa muonekano usio sawa.
Kwa mkristo ambaye anaye thamini ukristo wake sio mbaya kwenda na wakati(kuwa wa kisasa) lakini huo upya usiishie kwenye mavazi na mapambo katika mwili wako tu bali jitaidi hata katika utu wako wa ndani(mahali ambapo unaanda hatma yako katika Mungu) kwakua Roho mtakatifu anaweza akakupa hekima namna ya muonekano sahihi na kauli ya kuwajibu watu.
Ipetro 3:2-5,6-
Pamoja na hayo yote jua kuna nafasi ya wewe binafsi ya kujistiri kwakua wewe si kama mnyama hivyo unahitaji kuwa katika nafasi ambayo utaongeza marafiki na wala si maadui.
                                      

                                (a)Je! Nguo inawezekana kuwa tatizo katika ukristo.
Kwa upande wa Mungu hakuna shida kwakua mavazi yako haya mfichi Mungu asione utupu wako ila namna ya unavyo vaa inaweza kuwa tatizo kwa binadamu wanao kuzunguka.
Ni vizuri kutambua kuwa unapishana na watu na pia unakaa  na watu zaidi sana unawahitaji watu hivyo usipo wafanya wakufurahie jua kuna wakati utakapo wahitaji inawezekana historia ikasema ndani ya maisha yako.
Pindi unapokuwa sehemu Fulani kunautaratibu wake iwe ofisini,shambani n.k mathalani shuleni kuna namna utavaa kwa namna taratibu za shule zinavyo ruhusu na utavaa si kwamba unapenda kuvaa hivyo wakati mwingine inakulazim kuvaa hivyo kwakua unahitaji elimu na mambo mengi yaliyo mema.
Sikuzote tambua unaishi katika dunia ambayo uliwakuta watu wakiishi hivyo unapoenda nje ya utaratibu usitegemee jamii ikakukubali.
“mwanamke apaswi kuvaa mavazi yampasayo mwanaume”
Torati 22:5
Katika yote tunatambua kutokana na biblia inavyosema hakuna uhusiano ulio kati ya Nguo na Mungu isipokuwa Moyo wa mtu na Mungu ili ni muhimu kutangulia kulitambua.
Pamoja na hayo yote ni vizuri kuishi na watu vizuri na katika hali stahiki na pindi utakapo ona nguo ni kikwazo katika jamii badilika sio kwa sababu unawaogopa bali kwa sababu unawapenda wao na Mungu.
Waebrania 12:14
Tambua uwepo wa watu hao ndio unakupa umaana wewe kuwepo dunia peke yako itakuboa na haita leta maana na kufanya kuboreka. Hivyo jua unahitaji watu basi hakikisha uwepo wako ulete furaha kwao.
Usione ngumu kubadilika kwakua mazoezi mazuri yatakufanya uwe vizuri ukiamua unaweza, kwakua Mungu yupo kwa ajili ya kukuwezesha kuwa mtu wa maana mbele yake na hatimae mbele za wanadamu.(kwakua hakuna jambo la kumshinda Mungu).
Akili yako inahusika sana kwakua ndani ya akili ni ufunguo wa utendaji wako  hapa duniani akili ikibadilika basi ujue na wewe umebadilika.
Ni vizuri kutambua kuwa unao uwezo wakubadilika na jamii ikakukubali.
Paulo anasema…….
“nilivyoenda kwao nilikuwa kama wao”


Kwakua unatambua mavazi hayana ushirika na Mungu bali ni moyo wako na Mungu basi inawezekana kuacha mavazi ambayo ni kikwazo kwa watu wengi ila ukaendelea ukang’ang’ania ushirika wako na Mungu ndicho cha msingi kwako.
Ni vizuri kuhakikisha watu na Mungu wanafurahishwa katika uwepo wako.
“yesu akakua akimpendeza Mungu na wanadamu…….”
Luka 2:52
Ni kweli hata ukibadilika ukawa sawa na jamii unavyokutaka wako watu bado hauta pata kibali kwao ilo usijali ugomvi wachie Mungu na wao.

                                
                                         (b)Je! Nguo inamchango wowote katika kufanya ibada.
Ibada na nguo ni vitu viwili tofauti, nguo ni kwa ajili ya mwili tu na ibada ni jumla ya mambo yote yanaendelea ndani ya moyo wa mwanadam.
Japo mavazi yana maana mbalimbali kuna mavazi ambayo watu huona vema wayavae ofisini na kuna mavazi ambayo watu wanaona wa yavae sehemu za ibada na maeneo mengine kadili jamii husika ilivyoona vyema.
Hata katika biblia mavazi yalikuwa yana valiwa kutokana kazi husika, jinsia na hata rika gani linatakiwa livaeje?
-Watu walikuwa wanafua nguo ilikukutana na Mungu hivyo unadhifu na umaridadi ulikuwa unazingatiwa
Makuhani walikuwa na nguo(naivera) ambayo waliitumia katika kupeleka ibada kwa niaba ya wanaisrael.
Ni kweli nguo ni nguo na Mungu ni Mungu lakini pamoja na hayo unahitaji mambo ambayo yatakuwa msaada kwako katika kuimairisha mausiano kati yako na Mungu na binadamu;

Vaa nguo ambayo utaifurahia.
Vaa nguo ambayo itakuweka uwe huru ambayo haita toa staili ya kuenenda au kukaa jambo hili unaweza kuona ni jambo la kawaida lakini linaweza kukuweka kutofanya uhuru mbele za Mungu vilevile anahitaji mwili wake hutumie kwa ajili yako kwa maana hilo ni hekalu la Mungu.
I wakorintho 6:19
Ili ni ngumu kwa akili ya kibinadam unahitaji moyo utengenezwe na neno la Mungu ili uwe tayari kuyafanya hayo.( ni vizuri kujua kuwa unahitaji umfurahishe Mungu ili yeye akutane na mambo yako).
-ni muhimu kuvaa nguo ambayo haita kamata akili yako kiasi kwamba utashindwa kumwabudu Mungu na kumsifu yeye.
-vilevile hakikisha hiyo nguo isikupe mashariti jinsi ya kucheza kwa bwana.
Ukweli nguo si shida lakini inaweza kuchangia katika kuchafua moyo wako mwisho ikakupelekea kutoifurahia ibada napengine hata ukajuta kwanini umeivaa hiyo nguo.


                             (c)unafikiri Nguo inaweza kutoa picha ya mkristo(ushuhuda) kwa        waliookoka na wasio okoka.
Hata kama haitatoa au kutoa lakini ni vizuri uonye kuitambua jamii yako na kuipenda katika udhati.
Japo ni kweli kwamba hakuna kwa aina yoyote ya nguo ambayo yesu huitumia kufanya mambo yake bali mtu husika ndiye Mungu umtumia.
Na ni kwa uhakika vile ulivyo vaa ni vile ulijiona kuwa ndio muonekano ambao wewe unapendeza na kujikubali ndio ulivyo hili nalo ni muhimu sana. Hivyo kweli nguo ni pambo basi jipambe vizuri ujiletee kujikubali mwenyewe na wengine.


Kama nguo haitoi ushuhuda wa kristo kwanini kujadiliwa?
-unafikiri kwanini nguo(mavazi) yamekuwa yakijadiliwa na kuwa tatizo miongoni mwa watu walio okoka na hata wasiookoka. Pamoja na hayo limekuwa sababu ya kanisa la Mungu kuchafuliwa na kupoteza umaana na heshima yake.
-hivyo tunajadili kuondoa  hilo tatizo na hatimae heshima ya mwili wa kristo pale Mungu alivyokusudia. Japo tunaenda na wakati ni vizuri kwenda nao pasipo kuwa kwazo kwa wengine.
Ni muhimu sana kama mkristo ujue huko uliko jamii yako inatakaje ili hao wakufurahie na waone uthamani wa uwepo wako.
Na ni vizuri kupata uelewa na ujue jinsi gani ya kuishi kwa akili katika jamii uliopo ukijitahidi ili usiwe kwazo.
“mwenye akili siku zote upenda kuona watu wanafurahia hata kama kwake ni maumivu kwake”
Fanya mazoezi kwa ajili ya wewe binafsi kuongeza marafiki  na kujiongezea uhuru wako.

Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                     Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com



“UKIJUA NI VIZURI KUMJULISHA”




                                                                                                                                         

Jumatatu, 12 Agosti 2013

MAHUSIANO BAINA YAKO NA MUNGU KUWA YENYE NGUVU



HALI  YA  KUWA  WEWE NA MUNGU KUWA  YENYE  NGUVU                
                                        NDANI   YAKO:     

Ili mahusiano yoyote yawe na nguvu yanawategemea wahusika wenyewe wanavyo yafanya yawe na nguvu au yasiwe na nguvu. Kwa hakika hao ndio walio beba hatma yao yakuendeleza urafiki wao au la!           
              Yohana 15:13-15
    Daudi na Jonathan, sauli hakuweza kuutengenisha urafiki wao.
               Isamweli 18:1-4.
Katika urafiki kati yako na Mungu hiko wazi hauna tatizo bali tatizo liko upande wetu namna inakuwa shida kutokana mambo mbalimbali yanavyo tusonga, katika mambo hayo yako unayoshinda na mengine unashindwa.
                 Warumi 8:35.   
-japo sio kitu kizuri kusahau makubaliano yenu kwa kisingizio kuwa mambo mengi yanayo kukabili.
      
Kunamchanganuo ulio kati yako na Mungu wakuonyesha hali mliyo nayo.
                                    Mathayo 13:3-9

i.  zilianguka karibu na njia
ii. zilizoanguka kwenye miamba
iii. zilizoanguka kwenye miiba
iv. zilizoanguka kwenye udongo mzuri.

Hizi zote ni hatua waweza kutoka hatua moja kwenda nyingine kama ukiamua kutoka hapo na si vinginevyo.



I.zilizoanguka karibu na njia.
-ni mtu ambaye anajikuta anafuraha pasipo sababu, hatua hii mtu upenda sana kwenda kanisani ni hatua za awali uwa na furaha anapoona wakristo wenzake wakati mwingine ujisahau kuona kuwa hali aliyo kuwa nayo kuzani wote wana hali hiyohiyo.(ugeni wa ulimwengu mpya).
Hiki ni kipindi cha matazamio sio cha kudumu ntu yeyote wakati wowote chochote cha weza fanyika, anaweza akaona nyekundu imekuwa ya njano halafu akashindwa kuelewa.
-hii furaha muda wowote inaweza kuzimika.
       Mathayo 13:19

ii. zilizoanguka wenye miamba.
-ni mtu ambaye ameanza kutambua mambo yaliyomo ndani ya wokovu. Kuomba,kusoma neno la Mungu.(ufahamu wake kuanza kupata nuru ya Mungu,kuanza kupa upeo)
-ni mtu ambae anayeanza kuona kuwa neno la Mungu kuwa linaanza kuwa na nguvu ndani yake, na kuanza kuliamini neno la Mungu.(anayeanza kupata ufahamu kuwa kuna msubiri Mungu ili nae afanye katika maisha yake).
-ila mwisho ukosa uvumilivu endelefu.
     Mathayo 13:20-21

iii. zilizoanguka kwenye miiba
-hii hatua mtu alishaanza kufaidi matuda ya ki mungu, mtu alishaanza kuelewa na kutumika pamoja na Mungu. Hii ni hatua hatari sana kwani ujuaje, kujilinganisha uanzia hapo.
Kuona sasa anaweza hata lile amefanya kuhubiri, kuponya hajatambua kuwa hizi ni ishara ambazo zitaambatana na waaminio.
Hatua unaweza kujilinganisha na mtu yeyote ambaye mwanzoni ulikuwa una mweshim lakini sasa unaona mnalingana.
    Mathayo 13:22
Tatizo kubwa mtu huyu hazai matunda yaliyo na kibali kwa Mungu.

iv. zilizoanguka kwenye udongo mzuri.
-ni mtu aliye jitoa mwanga kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
Ni mtu ambaye ajui maana ya msamaha, upendo, uvumilivu, kiburi, asila, ubinafsi, kuchukuliana na mambo mengine kwakua anayeishi sio yeye bali kristo anafanyakazi.
Ni mtu aliye na nguvu ya kusimamia jambo katika maarifa na maongozi ya Roho mtakatifu.
-msingi mkubwa alio nao huyu ni nguvu ya kuelewa (kiwango cha juu cha kuelewa)
          Mathayo 13:23

Vitu vya kuimarisha:
I.uwezo wa akili yako kuyaelewa mambo ya mungu.
Hali hii upelekea kuwa na maarifa,akili njema.
Lazima uwe na tabia ya kutambua na kuelewa namna akili yako inavyoelewa mambo ya Mungu.

II.utayari wa kuyabeba ya Mungu
Wakati mwingine sio lazima uyaelewe mambo ya Mungu papo kwa papo bali uyakubali kama umepata kibali kwa uhakika anayeongea ni Mungu wala si kitu kingine.
-mariam katika kupokea ujumbe kutoka kwa malaika Gabriel
              Luka 1:26-33
-zakaria katika kuupokea ujumbe toka kwa malaika akiwa kama kuhani.
             Luka 1:8-15

III.ulinzi wa jambo lolote kabla ujaliluhusu kuwa na nafasi ndani yako.
Vile unavyo liruhu jambo ndani ya maisha yako ndivyo lina kutengeza wewe na kukupa sura yake. Mtu aliye na uchungu kuna kuwa na udhihirisho katika muonekano wake.
      Luka 5:43-45

Prepared by:
                    Cothey Nelson       -  0764 018 535 or Cotheyn@yahoo.com
                  
                    James Adili Katiti – 0713 398 042 or James.adili19@gmail.com


                                           

                                       “BARIKIWA ………SANA”
                                                                                                                       

Jumatatu, 5 Agosti 2013

KUWA MTUMISHI WA MUNGU

                             KUWA MTUMISHI WA MUNGU
Kumtumikia Mungu Kama apendavyo:
Ni jambo ambalo Mungu analitarajia litokee kwa mtu ambaye amemkubali kuwa yeye ni Mungu wake.
Waefeso 4:1-4
Wafilipi 1:27-29
Kwa hakika maisha ya ushindi mwelekeo sahihi wa kiMungu unakuja kwa usahihi ni pale tu utakapojua maana ya kumtumikia Mungu, na hii ni kawaida ya Miungu yote haiwezi kukufanikisha mpaka pale umeitumikia kwa namna inavyotaka yenyewe yani umewafanyia ibada ambayo wamekubali.
Wakolosai 2:6
Hili neno la kawaaida masikioni mwa watu wengi lakini kulisikia peke yake pasipo kueleweshwa na Mungu mwaenyewe ni ngumu kulielewa kwa namna yake.
Ukitaka kuupendeza moyo wa Mungu lazima ufikirie namna ya kufanya kitu mbele zake naye afurahie uwepo wako duniani.(hiki ndicho Mungu anakitaka kwako maadam ukishakielewa hiki hakuna kushindwa)
Na namna unavyomtumikia Mungu hicho ndicho kipimo sahihi namna unavyo mpenda.(kutumika kwa kupenda ni vizuri kwakua ni ishara ya kujua wajibu wako)
Kama kunakitu kikusumbue au kukinyime raha ni kutafuta namna ya kumtumikia Mungu kwa usahihi wake pasipo kushurutishwa wala kulazimishwa maana hapo ndipo palipo na ustawi wa maisha yako yaani chemchem isiyokauka, raha yako itokane baada ya wewe kutambua maana ya kumtumikia Mungu kuanza kumtukia Mungu.
Wafilipi 3:12
Sura ya Mungu,tabia zake,uwezo wake utaona kwa ukamilifu pindi utakapo kuwa ndani ya utumishi wake.
Kitu cha maana kwa Mungu ni wewe kuandaa mazingira ambayo Mungu atatenda kazi pamoja na wewe kwa namna yake.
Kama ukishindwa kutafuta na kujibidisha namna ya kumtumikia Mungu  sahau kuona mtembeo wa ki Mungu ndani ya maisha yako na una haja kujivunia katika wokovu.
Iwathesalonike 1:8-9
Hii ni siri pekee ya kukaa na miungu yoyote duniani ni kuitumikia na hakuna jambo linguine.
Nje  ya utumishi wa kweli mambo yote unayofanya hayana kibali kwa Mungu yaani kutoa,kuomba,kuimba n.k
Na maisha haya ndiyo yanakupa nguvu kusema mimi ni mali ya kristo kwa kuwa unamtukia yeye naye anayafurahia muungamaniko wenu.
Kumtumikia Mungu sio shida si kwasababu unaogopa jehanamu labda kuna urafiki kufanya jambo Kwa shirika lakini sio kumtumikia Mungu Kama apendavyo yaani una mtumikia Mungu Kama alivyo hakuna usaidizi mwingine.
.utendaji wa yesu ulitegemea Mungu anasemaje?
                                                     Yohana 8:29                         
Hakuna kitu kigumu kama kumtumikia Mungu katika matakwa yake yaani kufanya jambo kwa namna yake (vile awazavyo katika akili yake Mungu)
                                                        Luka 14:25-35, 17:33
                         
 I.hakuna kutoa hakuna kupata (no give no gain)                                  
 Japo hatutoi ili kupata bali ni kutekeleza maagano yetu kwake, ishara ya kuzingatia makubaliano yako na Mungu.
Maisha ni shamba japo si namna ya mwili bali katika roho, kama hauta toa hakiwezi kupata
-shamba lina sifa kubwa kupanda na kuvunwa, hivyo kama hakuna kupanda hakuna kuvuna hii ipo halisi sana.
Kutoa ni ishara kubwa sana kuwa Mungu anahusika na maisha yako hivyo unahusika na mambo yake kwa kutoa KWA AJILI YAKE.
Hili limekuwa jambo la adimu kwa watu wanaoenda kanisani kwa sababu ya kutembea mwilini au kutoa maslai binafsi kwanza.
Watu wengi hawaendi mbele kwa sababu hawajajua misingi halisi ya kutoa,wanatoa pasipo ukamilisho.
Lazima ujifunze kutoa fedha,muda,nguvu yako katika kuimarisha mwingiliano wako na Mungu. Utoaji wako mbele za Mungu hiyo ni ishara kubwa ya kumtegemea Mungu
Utoaji uliokamili inamaana kuwa moyo wako uko wazi kwa Mungu naye Mungu aweze kukupa kibali katika maisha yako.
Unapo penda kutoa muda wako,fedha na vitu vingine havina shida nabado unaona haitoshi sikuzote utafikiri namna ya kutoa zaidi ili akufurahie.
Usipotoa mwili wako kwa ajili Mungu tambua utatumika kwa ajili ya mambo mengine,magonjwa,mawazo yasiyo kuwa na maamuzi/yasiyo na muafaka wa kudumu na mambo mengi yatapata nafasi ndani yako.(ndoto za kubomoa ufalme wa Mungu ndani yako,uvivu katika mambo ya Mungu)
Hii ni ishara ya kujipima kwa Mungu ni namna gani unamjua,unamwitaji,thamni yako kwake hauhitaji kuweka mjadala kujitambua.
Kwakua Mungu alionyesha kukupenda pale tu alipotoa pumzi yake,uzima wake na hata mwanae wa pekee,kwaiyo utoaji ni msingi mzuri kuonyesha upendo.
                                                  Yohana 3:16
Kuwa na kitu wakati unae mpenda anakiitaji yupo hiyo si ishara ya kupenda hata kidogo(unayo nguvu,fedha n.k) huo ni unafiki wa kiwango cha mbele za Mungu,haimfurahishi Mungu na muda si mrefu utaona matunda ya kutomfurahisha Mungu(huwezi kutoka hatua moja kwenda nyingine kiafya,kiuchumi).
Usipojitoa usitegemee yeye kujitoa kwako.
                                               Wagalatia 6:7
 Prepared by,
                    Cothey Nelson  - 0764 018 535
                                                cotheyn@yahoo.com
                     
                      James katiti      -  0713 398 042
                                                james.adili19@gmail.com